UASISI WAKE:
Liliasisiwa kundi la viwanda la GIAD mnamo mwaka 1993 likiwa na lengo la kuleta muamko wa kiviwanda na wa kiteknolojiya zitakazoenea kila upande wa Sudan; ili waweze kufikia viwango vya uzalishaji katika eneo lote. Vile vile, shirika hili linalenga kuimarisha uzalishaji wa kiviwanda ndani ya nchi na kubuni miradi kwa lengo la kutaka kuboresha uchumi wa nchi kwa kutumia juhudi na uwezo wa nguvu watu iliyohitimu na iliyowezeshwa kitaaluma.
RUWAZA YETU:
Kuwa viongozi katika eneo kwa kutumia viwango bora vya uzalishaji vya kimataifa.
UWEZO WA KUNDI LA VIWANDA LA GIAD:
GIAD ina rasilimali na uwezo wa kitaalamu mkubwa aina anuwai; zikiwemo:
• Rasilimali ya watu waliohitimu na waliowezeshwa kitaaluma.
• Kazi za kiuhandisi bora na uwezo mkubwa wa viwanda na wa kuzalisha; kama vile:
Ustadi wa shirika na uwezo wake wa hali ya juu wa kubuni mbinu muafaka kwa kutumia programu za kisasa za kiuhandisi na pia kuwepo kwa maabara maalumu za kitaalamu.
Shirika linamiliki viwanda vya kisasa na vyumba spesheli vya kontroli, vifaa na mashini, vinavyotumia teknolojia mpya mpya za kisasa za kimataifa.
Kuna viwanda vya kuyeyusha na kuunda mapande ya vyuma.
Kuna uundaji wa paipu aina aina (za moja kwa moja, za mikunjo, nyembaba, nk.)
Kuna teknolojia tofauti tofauti za kisasa za uunganishaji wa vyuma; kama vile kuchoma kwa umeme au gesi nk.
Kuna tanuri maalum za kupakia rangi zinazotumia teknolojiya za kisasa.
Kuna vituo vya kufanyia ukarabati vilivyokamilika.
Kuna maabara aina aina za kisasa zilizokamilika.
SHUGHULI, UZALISHAJI NA HUDUMA ZA GIAD:
1. Bidhaa za umeme ( bidhaa za kielektroniki na vifaa vyake, vifaa na programu za mifumo ya umeme, nk).
2. Uundaji wa ndege; ikiwemo kuzidizaini, kuunda, kukarabati na kufunza.
3. Vyombo vya baharini; ikiwemo kuvidizaini, kuunda, kufunza na ukarabati.
4. Kazi za uchimbaji madini (utafiti, uchimbaji, kuchangia vyombo vya uzalishaji, kutoa huduma, kutoa suluhisho na ushauri ).
5. Ufuaji wa madini kama vile shaba, nyaya za aluminiam, pesa, medali za kila aina; ikiwemo kuzipa umbo, kuzitia rangi, nk.
6. Uundaji wa magari; yakiwemo magari madogo, malori, matrela, matanka, mashini nyenginezo nzito nzito, na vipuri vyao.
7. Uundaji wa vifaa vya kiukulima kwa wingi; matrakta, mashini zakulimia, mifumo ya unyunyizaji, uvunaji, na vifaa vya kudhibiti wadudu na maradhi ya makulima.
8. Vyombo vya usafiri; vya nchi kavu, baharini, na angani.
9. Nyanja za ujenzi wa majengo na miundo msingi :
Huduma za uchoraji wa ramani za ujenzi wa majumba, viwanda, mifumo ya umeme na ile ya kimekanikia.
Ujenzi wa miji ya viwanda.
Huduma za kiuhandisi za barabara na ishara za trafiki.
Kutayarisha na kujenga viwanda, pamoja na kutia mashini na vifaa vyake.
Kujenga, kutayarisha na kukarabati vituo vya kusambaza maji.
10. Teknolojiya ya angani:
Vyombo na vifaa vya kupokelea mawasiliano toka angani na kuchanganuwa data.
Uchoraji wa ramani na maelezo ya kijiografiya, ya kimazingira, ya kiukulima, na pia data za kijiolojiya.
Utayarishi wa stesheni za kukontrolia vyombo vya angani.
Kukuza uwezo wa ndani ya nchi wa kuunda madishi (tafiti za mustakbali).
11. Samani / Fanicha na vifaa vyake:
Fanicha za shule
Fanicha na vifaa vya hospitali
Vifaa vya kiofisi na vya kufundishia.
12. Kawi ya kudumu isiyoisha (miradi ya mustakbali):
Kawi hai (biofuel)
Miyale ya jua
Nguvu kawi ya upepo
Nguvu kawi ya maji
13. Idara :
Utekelezaji wa mifumo ya kisasa ya uwendeshaji wa idara.
Mifumo ya usimamizi ya kiteknolojiya, ya kiidara na ya kisheria.
Mifumo ya kuchunga usalama na uhifadhi wa mazingira.
Shahada za ubora za kimataifa zinazoafikiana na mifumo ya ubora ya Ulaya.
Mifumo ya ubora ya ujumla.
Mifumo ya kuendesha idara za nguvu watu.
Mifumo ya tarakilishi.
Kushajiisha ubunifu, talan